Isaiah 27:2-6

2 aKatika siku ile:

“Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:
3 bMimi, Bwana, ninalitunza,
nalinyweshea maji mfululizo.
Ninalichunga usiku na mchana
ili mtu yeyote asije akalidhuru.
4 cMimi sijakasirika.
Licha pangekuwepo michongoma na miiba kunikabili!
Ningepambana dhidi yake katika vita,
ningeliichoma moto yote.
5 dAu niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,
wao na wafanye amani nami,
naam, wafanye amani nami.”

6 eKatika siku zijazo, Yakobo atatia mizizi,
Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,
naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.
Copyright information for SwhNEN